Kocha wa Tottenham alia na mastaa wake

Kocha wa Tottenham alia na mastaa wake

Kocha wa Tottenham Hotspur Ange Postecoglou amesema timu yake imecheza vibaya ndiyo maana imepoteza dhidi ya Chelsea na hakuna sababu nyingine iliyochangia kichapo hicho.

Spurs ilikubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu England uliopigwa jana, ikiwa ni ishara kuwa timu hiyo ina wakati mbaya wa kumaliza kwenye nne bora.

Kocha huyo amesema anaona timu yake kwa sasa ipo kwenye wakati mgumu na ni lazima wahakikishe wanafanya juhudi za makusudi ili kumaliza kwenye nafasi nzuri msimu huu.

"Siyo ishu ya kwanini tumepoteza mchezo huu, nafikiri tatizo letu kubwa ni kuwa na matokeo mabaya mfululizo, kila siku matokeo yetu yamekuwa hayaridhishi, tumepoteza kwa Arsenal na leo kwa Chelsea, siyo matokeo mazuri kwetu, lazima tubadilike.

'Shida ni kwamba tunaruhusu mabao ya aina moja na baadhi ya wachezaji hawako sawa, kila siku tunafanya kazi mazoezini lakini makosa yetu yanakuwa yaleyale, nafikiri tunatakiwa kubadilisha baadhi ya mambo mazoezini ili tuwe kwenye mwenendo bora," alisema kocha huyo.

Spurs kwa sasa ipo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 60 ikibakiza michezo minne, huku Chelsea ikipanda hadi nafasi ya nane na pointi 51.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags