Kocha mpya Simba atinga na mambo matano

Kocha mpya Simba atinga na mambo matano

Kama tunavyojua ‘Klabu’ ya Simba kwa sasa bado haina furaha baada ya juzi kuendeleza ilipoishia kwa kuanza kinyonge Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ikilazimishwa sare ya bao 1-1, nyumbani na Asec Mimosas kutoka Ivory Coast huku ikionekana kucheza ‘soka’ chini ya kiwango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti limeorodhesha mambo muhimu matano, ambayo Benchikha anatakiwa kuyafanya katika msimu huu ili kurejesha furaha, ubabe na ufalme wa Simba katika ‘soka’ la Afrika.

USHINDI- Simba imepoteza hari ya kushinda ‘mechi’ siku hizi. Tangu imeifunga Ihefu bao 2-1 kwenye ‘mechi’ ya ‘ligi’ iliyopigwa Oktoba 28 mwaka huu haijashinda tena.

KUFYEKA NA KUSAJILI- Pili ni hili la kufyeka na kusajili wachezaji wapya, Kwa bahati nzuri Benchikha anaingia Simba kipindi ambacho dirisha dogo la usajili linakaribia kufunguliwa.

KUUNDA TIMU - Jambo la tatu ni kuunda ‘timu’ Unajua kuna kuwa na wachezaji wengi, wazuri, wabovu, bora na wakawaida, harafu kuna kuwa na ‘timu’ bora.

KUREJESHA MASHABIKI UWANJANI- Jambo la nne ni hili. Nilikuwepo juzi uwanjani wakati Simba na Asec zinacheza, katika miaka ya hivi karibuni Simba haijawahi kucheza ‘mechi’ ya kimataifa nyumbani huku jukwaani kukiwepo mashabiki wachache namna ile. Kwa Mkapa palipoa sana.

MATAJI- Jambo la mwisho ambalo linamsubiri Benchikha pale Simba na litamheshimisha zaidi ni mataji.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags