Klabu ya Al Hilal yavunja rekodi

Klabu ya Al Hilal yavunja rekodi

Klabu anayoichezea nyota wa Brazil Neymar ya Al Hilal kutoka Saudia imevunja rekodi ya dunia na kuingia katika kitabu cha ‘Guinness World Records’ baada ya kushinda michezo 34 mfululizo kati ya Septemba 2023 hadi Aprili 2024.

Timu hiyo ilishinda mchezo wao wa 28 mfululizo mwezi Machi kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya wapinzani wao Al-Ittihad na kuvunja rekodi ya 27 iliyowekwa awali na klabu ya Wales ya The New Saints mwaka 2016.

Rekodi hiyo ilifikia kikomo Aprili, 17, mwaka huu baada ya kufungwa bao 4-2 ugenini na timu ya Al Ain katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ya AFC.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags