Kiungo wa Real Madrid abeba tuzo ya Golden Boy

Kiungo wa Real Madrid abeba tuzo ya Golden Boy

Mchezaji wa ‘klabu’ ya #RealMadrid, #JudeBellingham ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi #Ulaya (Golden Boy) mwaka 2023.

 Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, anakuwa mchezaji wa tatu wa England kushinda tuzo hiyo akifuata nyayo za #WayneRooney aliyebeba 2004 na Raheem Sterling 2014. Bellingham amewashukuru waliompigia kura pamoja na ‘timu’ alizozichezea za #BirminghamCity, #BorussiaDortmund na #RealMadrid.

Hiyo ni tuzo kubwa kwa Bellingham ambaye ameanza kwa kishindo msimu huu akiwa na uzi wa Madrid. Msimu huu amefunga mabao 13 katika mechi 14 za kwanza akiwa na Madrid baada ya uhamisho wa Pauni 88.5 milioni kutoka Dortmund.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post