Kitambaa cha Jimi chapigwa mnada

Kitambaa cha Jimi chapigwa mnada

Kitamba cha aliyekuwa mwanamuziki wa Pop nchini Marekani #JimiHendrix ambacho alitumia kukivaa kichwani katika maonesho mbalimbali miaka ya 1960 chapigwa mnada wa tsh 100 milioni.

Inaelezwa kitambaa hicho kimeorodheshwa katika kumbukumbu za nguo ambazo msanii huyo alivaa katika matamasha yake, ambapo awali kilinadiwa kwa tsh 34 milioni katika mnada wa urithi wa  ‘Heritage Auctions’ nchini humo.

Jimi alifariki mwaka 1970 akiwa na umri wa miaka 27 pia aliwahi kuwa  na nyimbo kama ‘Hey Joy’, ‘little Wing’, ‘Foxy Lady’, ‘Purple Haze’, ‘Voodoo Chile’ na nyengine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags