Kitabu cha 2PAC kupigwa mnada

Kitabu cha 2PAC kupigwa mnada

Kitabu cha Mashairi cha 2Pac Kinatarajiwa Kupigwa mnada wa hadi $300,000, jumba la mnada Sotheby's linapiga mnada kitabu cha mashairi kilichoandikwa na msanii 2Pac alivyokuwa mdogo.

Rapper huyo aliandika kitabu hicho akiwa na umri wa miaka 11, na kukifanya kuwa kipande cha kwanza kabisa cha maandishi yake kwenye rekodi, nyumba hiyo ya mnada inasema Pac aliwazawadia kitabu hicho wafungwa wanne wa Black Panther, akiwemo the God father Jamal Joseph, ambaye alipatikana na hatia kwa kuhusika katika mauaji ya mwaka 1981 ya wizi wa gari la kivita la Brink.

Kitabu hiki kinajumuisha picha ya Pac akilala na kalamu mkononi, akiota kuhusu kuachiliwa kwa Black Panthers, alitia saini kipande, "Tupac Shakur, Future Freedom Fighter."

Forbes inaripoti kuwa kitabu hicho kinatarajiwa kufikia kiwango cha $200,000-$300,000, pia kitajumuisha barua za Pac zilizoandikwa kwa Mchumba wake, alipokuwa shule akiwa na umri wa miaka 17.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags