Kipa wa Brazil akwepa mpira makusudi

Kipa wa Brazil akwepa mpira makusudi

‘Golikipa’ wa ‘klabu’ ya #Corinthians ya nchini #Brazil, #CassioRamos, amewashangaza mashabiki wa ‘timu’ hiyo waliokuwa uwanjani baada ya kukwepa mpira uliopigwa langoni mwake.

Inaelezwa kuwa Cassio alisimama kwenye lango la ‘goli’ wakati ‘klabu’ ya Corinthians wakicheza dhidi ya ‘klabu’ ya #AtléticoMineiro, ambao walipata faulo ya Indirect Free Kick, iliyopigwa na mchezaji wa ‘timu’ ya Mineiro.

Lakini mwamuzi wa mchezo huo hakuruhusu bao hilo, kwa sababu ilikuwa ni free-kick isiyo ya moja kwa moja na hakukuwa na mchezaji mwingine aliyegusa mpira zaidi ya aliyeupiga.

Hata hivyo mashabiki walimpongeza mlinda lango huyo baada ya kuelewa alicho kifanya ilikuwa ni sheria ambazo ni muhimu kila mwanasoka kutambua.Mchezo huo ulimalizika kwa ushindi wa sare ya bao 1-1 kati ya ‘timu’ zote.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags