Kiongozi wa kundi la Morgan Heritage, Peetah afariki dunia

Kiongozi wa kundi la Morgan Heritage, Peetah afariki dunia

Mwanamuziki Peter Morgan maarufu kama Peetah, ambaye ni kiongozi wa kundi la Morgan Heritage la nchini Jamaica amefariki dunia siku ya jana Feb 25.

Taarifa ya kifo chake imetolewa kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa kundi hilo, ambapo licha ya kutoa taarifa hiyo hawajaweka wazi sababu ya kifo chake.

Morgan Heritage liliundwa mwaka 1994, likiongozwa na Peter Morgan(Peetah), likijumuisha ndugu watano, watoto wa msanii wa reggae Denroy Morgan akiwemo Una Morgan, Roy ‘Gramps’ Morgan, Nakhamyah ‘Lukes’ Morgan, na Memmalatel ‘Mr Mojo’ Morgan.

Peetah akiwa kwenye kundi la Morgan Heritage alifanikiwa kushirikiana na wasanii mbalimbali wa Tanzania akiwemo DiamondPlatnumz kwenye wimbo wake wa 'Hallelujah', Harmonize wimbo 'Malaika' na RomyJons wimbo 'Ready'.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags