King Majuto alikuwa sanaa kamili

King Majuto alikuwa sanaa kamili

Furaha ndiyo kila kitu kwa maisha ya mwanadamu. Tunatafuta pesa ili kujenga furaha. Tunataka uongozi bora ili tuwe na furaha. Tunaoa, kuolewa na watu sahihi ili tuishi kwa furaha.

Kila kitu kinafanyika ili kuleta furaha, kazi ya kutengeneza furaha kwenye mioyo na nyuso za binadamu, King Majuto alifanya kwa miaka mingi sana bila kutuangusha hata mara moja. Mpaka mwili wake unaacha roho aliendelea kuwa kiwanda cha kuzalisha furaha.

Msanii mmoja aliniambia kuwa Mzee Majuto alifanya naye kazi nyingi. Lakini ndiye msanii ambaye alimpa tabu sana. Tabu ya kuvumilia kumaliza 'sini'. Yaani 'sini' moja wangerudia mara kumi kwa sababu ya kushindwa kuzuia kicheko kwenye jambo 'siriazi'.

Kila kitu alichofanya Mzee Majuto kilikuwa kicheko kwa wengine. Pengine mtu pekee aliyemzoea ni mkewe na mama yake mzazi. Sisi wengine ilikuwa ngumu kumzoea. King Majuto alikuwa sanaa kamili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags