Kinachoendelea kwa Kapteni aliyedondoka uwanjani

Kinachoendelea kwa Kapteni aliyedondoka uwanjani

Nahodha wa ‘klabu’ ya #LutonTown, #TomLockyer ambaye alidondoka uwanjani jana kutoka na matatizo ya moyo wakati ‘timu’ yake inacheza dhidi ya ‘timu’ ya #Bournemouth na kusababisha mchezo ughairishwe kwa sasa anaendelea vizuri.

 Dakika moja baada ya ‘timu’ ya #Bournemouth kusawazisha na ubao kusoma 1-1, Lockyer alidondoka kwenye nusu ya uwanja wa eneo lao ambapo ilisababisha mtafaruku hata ‘mechi’ ikagharishwa kwa sababu wachezaji walikataa kucheza kwa kuwa hawakuwa sawa kiakili kutokana na tukio hilo.

‘Kocha’ wa Luton Rob Edwards mara tu baada ya Lockyer kudondoka aliingia uwanjani akifuatiwa na wachezaji sambamba na madaktari wa timu zote mbili walifika kumpa huduma ya kwanza.

Taarifa kutoka daily Mail zinadai ‘staa’ huyo kwa sasa anaendelea vizuri baada ya matibabu, pia picha mbalimbali zilimuonesha akiwa na wachezaji wenzake waliomtembelea hospitalini.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags