Kilichomkimbiza Ray C Tanzania

Kilichomkimbiza Ray C Tanzania

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Rehema Chalamila maarufu Ray C ameweka wazi kuwa sababu ya kuondoka Tanzania na kuhamia Paris, Ufaransa ni kutokuwa sawa kiafya.

Ray C amesema kuwa alipitia kwenye matatizo makubwa kwa hiyo alihitaji kupona kiroho ndiyo maana akaondoka.

“Nilipitia matatizo, mtihani mkubwa sana lakini namshukuru Mungu kwamba niliweza kusimama tena mwaka 2017/18 nikarudi tena studio nikaanza kurekodi, kufanya kazi na kutoa nyimbo lakini bado nilikuwa nahitaji kupona kwenye moyo.

"Unajua unaweza kupona tu physical lakini moyo bado una mambo mengi kwa hiyo nikasema mimi ili nipate amani ya moyo inabidi niondoke kwa sababu tayari nilishaanza kuona watu hawanichukulii serious, sawa nilikuwa nafanya vizuri lakini sikuona ile thamani",amesema.

Aidha amesema aliamua kuondoka nchini ili awashangaze waliokuwa wanamdharau.
"So wakati najitafuta ndiyo nikaona mimi nitoke kwa sababu mimi nishatoka sana nikapiga goti kwa Mungu, kumuomba anitoe kwenye hii nchi nikatulie, nikapone kiimani ili wale waliokuwa wakinidharau waone ukuu wako na kweli Mungu amefanya,” amesema Ray C.

Utakumbuka kuwa Ray C aliwahi kutamba na ngoma kama ‘Uko Wapi’, ‘Mama Ntilie’, ‘Umenikataa’, ‘Touch Me’, ‘Sogea Sogea’ na nyinginezo kibao.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post