Kilicho mkondesha Post Malone ni soda sio madawa ya kulevya

Kilicho mkondesha Post Malone ni soda sio madawa ya kulevya

Mwanamuziki wa Hip-hop kutoka nchini Marekani Post Malone amewajibu mashabiki waliyoshangazwa na kupungua kwa mwili wake, na kudai kuwa msanii huyo anatumia madawa ya kulevya ndiyo maana anaonekana kupungua mwili kwa kiasi kikubwa.

Post Malone ambaye kwa sasa ni baba wa mtoto mmoja aliyempata hivi karibuni amedai kuwa kupungua kwake hakuhusiani na madawa ya kulevya kwani hayatumii, bali amepungua kutokana na malezi ya mwanaye kwasababu ndiyo mara yake ya kwanza kuwa baba.

Hakuishia kutoa sababu hiyo tu pia amedai kuwa kwa sasa ameacha kunywa soda na vyakula vyenye sukari kwa wingi kwani ndivyo vilikuwa vikisababisha awe na uzito mkubwa huku akidai kuwa kwa sasa anakula vyakula vya kujenga mwili wake ili aishi maisha marefu ya kumlea mtoto wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags