Kila kilichoibiwa kitapatikana

Kila kilichoibiwa kitapatikana

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limeendelea kufanya operesheni ya Mtaa kwa Mtaa katika maeneo ya Bunju A na B na kufanikiwa kuwakamata Watu sita wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu (Panya Road) huku likisema vitu vyote vilivyoibwa vitapatikana.

Akizungumza usiku wa kuamkia leo katika Kituo cha Polisi Mabwepande Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema Watuhumiwa hao baadhi yao wamekamatwa katika maeneo ya Mapinga Bagamoyo mpakani pamoja na kufanikiwa kukamata baadhi ya vitu walivyoiba ikiwemo simu.

“Nitoe onyo Panya Road hawa wakijitoa ufahamu wakajaribu kushambulia Askari Polisi, Polisi watajihami na watajihami kwa kutumia nguvu inayolingana na mashambulizi na aina silaha wanazozitumia”

“Malengo yetu ni kuhakikisha kila kitu kilichoibwa kwenye tukio hili kinapatikana lakini kuhakikisha kila aliyehusika kwenye tukio hili anaingia kwenye msukosuko mkubwa wa kisheria na kuhakikisha wanafikishwa Mahakamani”

haya mdau dondosha comment yako hapo kuhusiana na sakata hilo na kauli aliyoitoa kamaanda wewe unasemaje hapo?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags