Kikongwe zaidi duniani apoteza maisha

Kikongwe zaidi duniani apoteza maisha

Mwanamke aitwaye Maria Branyas Morera kutoka Hispania ambaye alikua akishikiria rekodi ya dunia ya ‘Guinness World Records’ kuwa binadamu mzee zaidi amefariki akiwa na umri wa miaka 117.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na familia ya kikongwe huyo siku ya jana Agosti 20, 2024 katika mtandao wa X (zaman twitter) wakieleza kuwa mwanamke huyo amefariki kwa amani akiwa usingizini.

Branyas Morera alizaliwa San Francisco Machi 4, 1907, alithibitishwa kuwa mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi Januari 2023 baada ya kifo cha aliyekuwa akishikiria rekodi hiyo Lucile Randon, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 118.

Hata hivyo kwa mujibu wa Guiness binadamu ambaye aliweza kuishi miaka mingi zaidi ni Jeanne Louise Calment kutoka Ufaransa ambaye alifariki mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 122 na siku 164.

Aidha kwa sasa nafasi hiyo inaweza kuchukuliwa na Tomiko Itooka kutoka Japan, ambaye alizaliwa Mei 23, 1908 ana umri wa miaka 116, kulingana na Utafiti wa Gerontology wa Marekani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags