Kijana wa miaka 15 azindua sabuni ya kutibu saratani ya ngozi

Kijana wa miaka 15 azindua sabuni ya kutibu saratani ya ngozi

Kijana mmoja aitwaye Heman Bekele (15) kutoka Fairfax, Virginia ameripotiwa kuvumbua sabuni inayoweza kuzuia na kutibu saratani ya ngozi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa mtoto huyo alianza harakati zake za uvumbuzi toka alipokuwa mtoto nchini Ethiopia, baada ya kuona athali kubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambao wanasumbuliwa na saratani ya ngozi.

Ingawa bado iko katika hatua za awali ambapo inaweza kuchukua miaka kadhaa kabla ya bidhaa hiyo kuingia sokoni. Hata hivyo msimu huu wa joto Heman kila siku moja ya wiki anaitumia kufanyakazi katika maabara ya Shule ya Afya ya Umma ya Johns Hopkins Bloomberg ili kutimiza ndoto zake.

Aidha kwa mujibu wa maelezo ya kijana huyo ameweka ahadi kufanya matibabu ya saratani ya ngozi yapatikane kwa urahisi na gharama nafuu ulimwenguni kote hasa kwa jamii ya watu wasiojiweza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags