Kijana akamatwa kwa kupigana na mzee wakigombania kiti

Kijana akamatwa kwa kupigana na mzee wakigombania kiti

Kijana wa miaka 27, Jesse Montez Thorton atiwa mikononi mwa polisi kwa kupigana na mzee wa miaka 63 wakati wakigombania kiti kweye Ukumbi wa Sinema uliopo Pompano Beach, Florida.

Inaelezwa kuwa mzee huyo alimkuta kijana huyo akiwa amekaa na mwanamke kwenye kiti, na kumuomba anyanyuke kwa madai ya kuwa ni viti vyake kwani alikata ‘tiketi’ ya viti viwili, kimoja chake na kingine cha mke wake.

Hata hivyo inadawa kitika mabishano ya kugombania kiti hicho kijanaa huyo alisimama na kumrushia ngumi mzee huyo na kupelekea adondoke hadi kupata majeraha kichwani na usoni.

Baada ya kutekeleza tukio hilo kijana huyo aliondoka akiwa ameongozana na mwanamke aliyekuwa amekaa naye, lakini kufuatia video mbalimbali za tukio hilo zilizokuwa zikisambaa, kijana alifanikiwa kukamatwa na polisi wa Fort Lauderdale na hadi sasa yupo kwenye Gereza Kuu la Kaunti ya Broward.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags