Kifo cha MohBad kitendawili, ‘Voice note’ yasambaa shuhuda afunguka

Kifo cha MohBad kitendawili, ‘Voice note’ yasambaa shuhuda afunguka

Kutokana na kuwepo kwa tetesi za aliyekuwa msanii wa muziki nchini Nigeria MohBad kufikishwa kwenye hospitali ya Perez Medcare akiwa amefariki, kwa mujibu wa taarifa kutoka katika hospitali hiyo.

Lakini kumeendelea kuwa na sintofahamu mbalimbali juu ya kifo cha msanii huyo baada ya kujitokeza mmoja wa mashuhuda nchini humo kukanusha akidai MohBad alifikishwa akiwa mzima.

Shuhuda huyo amekanusha kupitia voice note inayosambaa mitandaoni akieleza tukio lilivyokuwa hospitalini hapo.

Aidha shuhuda huyo anaeleza kwenye voice note hiyo kwa kudai alishuhudia MohBad akiwa hai lakini katika hali ya kuzidiwa akifikishwa kwenye hospitali ya Perez Medcare.

Majira ya asubuhi ndipo baada ya kumuona MohBad alishituka na kumuomba apige naye picha huku akimuueleza kuwa yeye ni mmoja wa mashabiki wake.

Katika madai ya shuhuda huyo amesema kuna ‘nesi’ alifanya naye mazungumzo na akadai kuwa amemchoma MohBad sindano.

Lakini baada ya muda kidogo aliona rafiki ambaye aliongozana na msanii huyo ghafla alitoka na mwili wa Mohbad huku akipiga kelele.

Ikumbukwe MohBad alifariki tarehe 12 ya mwezi huu, baada ya kutoka kwenye show Ikorodu nchini humo na kuzikwa siku ya pili lakini kutokana na utata wa kifo chake mwili wake ulifukuliwa kwa uchunguzi zaidi ikiwa bado uchunguzi huo hajaleta majibu hadi sasa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags