Mchekeshaji Kicheche amewataka wachekeshaji waachane na tabia ya kujipendekeza kwa wasanii wa muziki kwa sababu wanakuwa kama chawa wa wasanii hao huku hakuna kitu wanachonufaika zaidi ya kuonekana kwenye video.
Kicheche amedai kuwa wanachohitaji kutoka kwa wasanii ni nguvu ya support na sio kuwaona kama vituko kwani kuwaona hivyo ni kushusha thamani ya sanaa ya uchekeshaji.
Licha ya kusema hayo mchekeshaji huyo akaongezea kuwa wachekeshaji hawana ushamba wa kuwaona wanamuziki, kwani yeye anamaauzi yake kama mwanamuziki akimuhitaji kwenye kazi yake, kwenda ama kutokwenda inategemea huyo msanii kamfuata kwa namna gani.
Leave a Reply