Na Asha Charles
Staa wa muziki wa Taarabu nchini, Khadija Kopa amefunguka na kuwataka wasanii wenzake waweze kujikita katika shughuli za kijamii.
Akizungumza na moja ya chombo cha habari nchini, mwanamuziki nguli wa nyimbo za mwambao Khadija Kopa amenukuliwa akisema, “Yaani mimi natamani hizi NGO’s (mashirika kutoka nje) zishirikiane na sisi wasanii kwa ajili ya kuhamasisha na kufanya promotion kuhusu watoto njiti ili watu waweze kujua. Kwa maana wengi wao hawajui kuhusu watoto njiti,” amesema Khadija Kopa.
Aidha, Malkia huyo wa Mipasho alielezea kuhusia na wasanii kutunga nyimbo ili suala hilo liwe jepesi kuwafikia watu kwa haraka. Siku zote ustaa lazima uhamasishe jamii kwenye shughuli mbalimbali.
Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka nchini Tanzania asilimia 17 ya watoto huzaliwa kabla ya muda wa mimba kukomaa (njiti).
Khadija Kopa na waimbaji wengine wa muziki wa taarabu akiwemo Leilay Rashid na Sabaha Salum Muchacho wanatarajia kuandaa matamasha maalumu kwa ajili ya kurudisha furaha kwa kina mama waliojifungua watoto kabla ya wakati (njiti).
Leave a Reply