Khaby Lame, Kinara wa Tiktok

Khaby Lame, Kinara wa Tiktok

Wewe mwenzangu na mie ukihangaika na vifollowers vyako 100 wenzako huku wanashikilia nafasi za juu za kuwa na wafuasi wengi (followers)

Raia wa Senegal Khaby Lame ametajwa kuwa ndiye Mtu mwenye wafuasi(followers) wengi zaidi wanaomfuatilia katika mtandao wa TikTok duniani.

Khaby Lame, ambaye anatumia jina la @ khaby.lame, amempiku Mmarekani Charli D'Amelio  ambaye alikuwa akishikilia nafasi  hiyo tangu mwaka 2020, Lame amefikisha wafuasi(followers) milioni 142.7 kwa usiku mmoja akiwa mbele ya Charli D'Amelio ambaye ana wafuasi(followers) 142.3.



Lame alizaliwa Senegal na familia yake ilihamia Chivasso, Italia akiwa na umri wa miaka 1, alifungua akaunti yake ya TikTok na kuchapisha video yake ya kwanza Machi 2020, baada ya kuachishwa kazi kiwandani siku za mwanzo wa janga la COVID-19.

Vichekesho vya kijana huyu vimepata ufuasi mkubwa na amekuwa mmoja wa watengeneza maudhui wanaotambulika na kupendwa TikTok ulimwenguni, amejizolea umaarufu kwa aina yake ya uchekeshaji wa bila kuongea neno lolote zaidi ya ishara za usoni na lugha ya vitendo (video zake kwa kawaida hazijumuishi mazungumzo) zimeruhusu maudhui yake kuvutia ulimwenguni pote.

Haya wadau wa mwananchiscoop haya tuambie mwenzetu uko na followers wangapi au nikuache kwanza, dondosha koment yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags