Kerry afahamu anayeishi naye si baba yake mzazi akiwa na miaka 41

Kerry afahamu anayeishi naye si baba yake mzazi akiwa na miaka 41

Muigizaji Kerry Washington mwenye umri wa miaka 46 afunguka kufahamu ukubwani kuwa baba anayeishi naye siyo baba yake mzazi.

Kerry amedai kuwa aligundua hilo mwaka 2018 baada ya kuwashirikisha wazazi wake kuwa amepanga kuonekana kwenye Tv show ya “Finding Your Roots” ya Henry Louis Gates Jr ambayo watu mashuhuri hujifunza kuhusu mababu zao kwa kupima DNA.

Baada ya kuwashirikisha hilo ndipo wazazi wake walimualika nyumbani na kumueleza ukweli kuwa alikuwa ni mtoto aliyepatikana kwa upandikizwaji wa mbegu za mwanaume mwingine, baada ya wazazi hao kutafuta mtoto kwa njia ya kawaida bila mafanikio.

Hata hivyo Kerry amedai kuwa jina la mtu aliyetoa mbegu zake halikufahamika.

Kutokana na hilo muigizaji huyo ameamua kuandika kitabu kiitwacho ‘Thicker Than Water’ kilichotoka leo kikielezea maisha yake.

Japo kwa upande wa wazazi wake hawakupenda aeleze kuhusu kulelewa na baba asiyekuwa baba mzazi, na kudai kuwa walipanga kutomwambia kamwe jambo hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags