Kayumba apokea mualiko kutoka kwa mwana fa

Kayumba apokea mualiko kutoka kwa mwana fa

Baada ya ku-share taarifa kuhusiana na kudai kuwa amedhurumiwa tsh 7 milioni na Rayvanny pamoja na Director Erick Mzava, na sasa mwanamuziki huyo amedai kuwa amepata mualiko kutoka kwa Waziri MwanaFa kwa ajili ya kupata muafaka wa suala hilo.

Kayumba kupitia ukurasa wake wa instagram ame-share picha akiwa pamoja na MwanaFa iliyoambatana na ujumbe uliokuwa ukieleza kuwa siku ya leo Februari 22 amepokea wito kutoka kwa Waziri MwanaFa kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ambapo walipata wasaa wa kuzungumza ili waweze kupata muafaka wa namna nzuri ya kupata haki yake.


Aidha mwisho kabisa Kayumba alitoa shukrani zake kwa Wizara ya Sanaa kwa kum-sapoti, na kumalizia kwa kueleza kuwa mambo yote ameikabidhi Serikali.
.
.
#mwananchiscoop
#burudikanasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags