Kariakoo ya Maua Sama yafutwa youtube

Kariakoo ya Maua Sama yafutwa youtube

Mwanamuziki Bongo Fleva nchini Maua Sama alia na watu ambao wameushusha wimbo wake wa ‘Kariakoo’ uliokuwa ukifanya vizuri katika mtandao wa Youtube.

Maua muda mchache uliyopita ameshare taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiandika kuwa ‘Kwahiyo mmkaamua kuishusha Kariakoo kule YouTube?, nimekosea nini?”, ameandika Maua Sama.

Wimbo wa Kariakoo uliachiwa rasmi siku mbili zilizopita ambapo aliwashirikisha mastaa wenzie akiwemo Jaiva, Ibraah na G Nako huku ukiandaliwa wa mtayarishaji anayetamba kwa sasa S2kizzy ‘Zombie’.

Kwa sasa kupitia mtandao wa Youtube wa mwanamuziki huyo wimbo wa mwisho ni ‘Poa’ uliotoka miezi miwili iliyopita huku akimshirikisha Nandy.
.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags