Kapteni Edward Smith wa Titanic Afariki dunia

Kapteni Edward Smith wa Titanic Afariki dunia

Mwigizaji maarufu kutoka nchini Marekani Bernard Hill, ambaye alitambulika zaidi kupitia filamu ya Titanic amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.

Taarifa ya kifo chake ilithibitishwa na wakala wake, Lou Coulson kupitia ukurasa wake wa Instagram huku sababu ya kifo chake ikiwa haijawekwa wazi. Hill alicheza uhusika kwa Kapteni katika filamu ya Titanic akitambulika kwa jina la ‘Kapteni Edward Smith’.

Bernard Hill alizaliwa Desemba 17, 1944 Blackley, Manchester, Uingereza na alipata umaarufu kupitia filamu kama ‘ParaNorman', 'The Kid', 'The Lord of the Rings: The Return of the King',  'Titanic', 'The Scorpion King' na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post