Kanye West kikaangoni, Vazi la kufunika uso lamponza

Kanye West kikaangoni, Vazi la kufunika uso lamponza

Rapper Kanye West, ameendelea kuwekwa kikaangoni nchini Italy kutokana na matukio yake, awamu hii mkali huyo anashutumiwa kwa kuvunja sheria za Italy za kupambana na ugaidi.

Shutuma hizo zimekuja mara baada ya Kanye kuvaa vazi lililofunika mwili mzima huku likiacha sehemu ndogo ya macho jambo ambalo si ruhusa nchini humo.

Kanye West alionekana Milan akihudhuria onesho la mitindo la Zanotti huku akiwa amevalia vazi hilo jeusi lenye kuficha mwili wake jambo ambalo ni kinyume na sheria za kupinga ugaidi ambayo hairuhusu mtu kuvaa kitu chenye kuficha utambulisho wake.

Isipokuwa kwa sababu za kidini tena kwa kibali maalum kwa watu wanaokiuka sheria hiyo hutakiwa kulipa faini kuanzia Euro 1,000 hadi 2,000.

Hata hivyo siku si nyingi Kanye West na mkewe Bianca Censori, walipigwa marufuku maisha yao yote kutumia ‘boti’ za moja ya kampuni iliyopo nchini humo baada ya kufanya vitendo vya kukiuka maadili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags