Kanye West apitia wakati mgumu kutoa albamu yake

Kanye West apitia wakati mgumu kutoa albamu yake

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Kanye West anadaiwa kupata tabu katika harakati zake za kuachia ‘albamu’ yake mpya baada ya ‘lebo’ za muziki nchini humo kumkwepa kutokana na kauli yake aliyoitoa mwaka jana juu ya taifa la Israel.

Tovuti ya Billboard imeeleza kuwa licha ya ‘albamu’ hiyo kuwa tayari imekamilika lakini wamiliki wa ‘lebo’ nchini homo hawataki kushirikiana naye kwenye kuisambaza ‘albamu’ hiyo kutokana na kauli yake aliyoitoa pia hawaoni kama ina nyimbo nzuri zitakazovutia.

Mwaka jana Kanye alitoa kauli iliyoashiria chuki kwa Waisrael juu ya mgogoro wao unaondelea dhidi ya Palestina. Hata hivyo aliomba msamaha juu ya kauli zake hizo alipofanya mahojiano na Piers Morgan.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags