Kanye ashitakiwa kwa unyanyasaji

Kanye ashitakiwa kwa unyanyasaji

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani #KanyeWest amefunguliwa mashitaka na aliyekuwa mfanyakazi wake wa zamani katika shule yake ya ‘Donda’ iliyopo Los Angeles, kwa ubaguzi na unyanyasaji.

Mfanyakazi huyo aliyetambulika kwa jina la Trevor Philips amedai kuwa Kanye alikuwa akiwafokea walimu wenye ngozi nyeusi na kutopaza sauti kwa waliupe weupe.

Philip alifundisha katika shule hiyo ndani ya mwaka mmoja ambapo mwaka 2023 alifukuzwa kazi baada ya msanii huyo kutaka kumsweka jela kwa sababu ya kusimamia haki zake.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2022 Kanye aliwafukuza walimu wawili shuleni hapo na baadae walimu hao walimshitaki na kufichua baadhi ya mambo yaliyokuwa yakiendelea katika shule hiyo kama wanafunzi kula mlo mmoja kwa siku, kusimama wakati wa masomo, pamoja na kulazimishwa kuvaa mavazi meusi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags