Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma, Kanali Michael Ngayalina ametoa onyo kwa watendaji wa kata na viongozi wa Serikali katika wilaya hiyo kutobeba michepuko katika magari na pikipiki za Serikali kinyume na matumizi ya vifaa hivyo na kwamba akibainika mtu amebeba michepuko atachukuliwa hatua za kisheria.
Kanali Ngayalina ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi vifaa hivyo ambaoo amesisitiza utunzaji na matumizi yenye tija ya vifaa hivyo vya usafiri ili kuleta matokea chanya kwa wananchi.
"Vifaa hivi visibebe michepuko. Mimi lile gari nimepewa na Serikali, linafanya shughuli ya Serikali, nikionekana nimebeba michepuko kila siku na lile gari nadhani wote mtanidharau na hamtoniheshimu."
"Kwa hivyo wale mtakaopewa hivi vyombo msibebe michepuko na tunajuana na huenda mwingine anaweza kwenda kutamba na kusema hii pikipiki ni yangu."
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Serikali imetoa magari matatu likiwemo lori kubwa pamoja na pikipiki tisa vyenye thamani ya Tsh. Milioni 427 ambapo Watendaji wa Vijiji 7 wamepatitwa usafiri wa pikipiki ili kuongeza tija katika utekelezaji wa miradi pamoja na ukusanyaji wa mapato,” alisema Ngayalina.
Leave a Reply