Kampuni ya Musk imeanza kupandikiza chipu kwenye ubongo

Kampuni ya Musk imeanza kupandikiza chipu kwenye ubongo

Na Sute Kamwelwe

 Wakati teknolojia ikizidi kukua siku hadi siku kampuni ya tajiri nambari mbili duniani Elon Musk iitwayo Neuralink imesema imefanikiwa kupandikiza kifaa cha kiteknolojia (Chip)  kwenye ubongo wa binadamu.

Ingawa hajatoa maelezo kamili ya mgonjwa wala kifaa hicho ila inatajwa kuwa ni hatua muhimu kwa kifaa kinachoitwa ‘Telepathy’, chenye uwezo wa kumruhusu binadamu kutumia simu au kompyuta kwa njia ya kufikiria.

"Binadamu wa kwanza amepokea kipandikizi kutoka Neuralink jana (juzi) na anaendelea vizuri," Musk amesema katika chapisho kwenye mtandao wa X.

Ikumbukwe kampuni hiyo ilipokea idhini kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), kwaajili ya kufanya jaribio lake la kwanza mwaka jana ambapo ilitangaza kutafuta watu wa kujitolea kupandikizwa.

Kupitia Neurotechnology iliyoanzishwa na bilionea huyo mwaka 2016 kampuni hiyo inalenga kujenga njia za mawasiliano ya moja kwa moja kati ya ubongo wa mwandamu na kompyuta.

Shirika la Habari la AFP limesema matarajio ya kampuni hiyo ni kuongeza uwezo wa binadamu, kutibu matatizo ya neva kama vile ALS au Parkinson, na kufikia uhusiano wa kimaelewano kati ya binadamu na akili bandia.

Musk ameongeza kwamba watumiaji wa awali watakuwa wale ambao wamepoteza matumizi ya viungo vyao maanayake ni kuwa itawawezesha watu waliopooza kutumia simu zao za kisasa kwa akili zao haraka na bila kutumia vidole. Tovuti ya Mint imeandika.

Hata hivyo, Neuralink tayari imefanya majaribio ya kina kupandikiza chipu kwa wanyama wakiwemo Nyani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags