Kampuni ya Apple yaupiga mwingi

Kampuni ya Apple yaupiga mwingi

Kwa mara ya kwanza Kampuni ya Apple inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya mawasilia imeshika nafasi ya kwanza kuwa mtengenezaji mkubwa wa simu za mkononi duniani kwa mwaka 2023.

Takwimu hizo zilizotolewa Januari 15, na Shirika la Kimataifa la Data (IDC), imeripoti kuwa kampuni hiyo kwa mwaka 2023 ilisafirisha simu milioni 234.6 na kupata hisa asilimia 20.1 huku Samsung ikisafirisha simu milioni 226.6 na kupata hisa asilimia 19.4.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kampuni ya Sumsung kupoteza katika mauzo ambapo alishikilia nafasi hiyo kwa miaka 13. Huku simu nyingine ambazo zimeingia katika tano bora zikiwa ni Xiomi, OPPO na Transsion.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags