Kamera za nini mnapoenda kutoa misaada

Kamera za nini mnapoenda kutoa misaada

Kitaa kinasema siku hizi ukitaka kusaidiwa kubali kuonekana kwenye mitandao ya kijamii, kuwa umepokea msaada.

Zile mbwembwe wanazofanya wakienda vakesheni na bebe zao, ndizo wanafanya pia kwa watu wanaowapatia misadaa, kamera nyingi za kupiga picha na kuchukua video, kila wanachotoa na anayepokea.

Siku hizi, wanaoenda kutembelea kwenye vituo vya watoto yatima na wasiojiweza, bila kupiga picha na kuposti hawaoni kama wamefanya wema.

Balaa lipo wakifika kwenye mitandao ya kijamii, wana andika kapsheni ndefu za kutia huruma na kujinadi kuwa wametoa misaada.

Ukizama kwenye vitabu vya dini vinasema ukitoa mkono wa kulia, wa kushoto usijue.
Hivyo basi mitaa inauliza, kuna ulazima wa kupiga picha na kuchukua video watu mnaowapa misaada?

Picha iliyotumika kwa msaada wa Akili Bandia






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post