Kajala akubali yaishe, Aomba radhi kwa mzazi mwenziye Majani

Kajala akubali yaishe, Aomba radhi kwa mzazi mwenziye Majani

Mwigizaji Kajala Masanja amemuomba radhi mzazi mwenziye Paul Matthysse maarufu kwa jina la 'P Funk Majani' kutokana na migogoro waliyokuwa wakipitia kwa muda mrefu.

Kajala ameomba msamaha huo usiku wa kuamkia leo katika sherehe ya kufichua jinsi ya  mtoto mtarajiwa wa Paula Paul na Marioo(Omari Ally ). Wakati akiomba msamaha huo ameeleza kuwa kwa muda wamekuwa wakiomba msaada kwa Majani kupitia mkewe kutokana na wao kutokuwa na maelewano.

"Napenda kumshukuru Paul kwa kuelewa, kuna vitu vingi sana alikuwa anaenda 'agensti' hapendi vinavyoendelea kama baba na mimi nilikuwa najua kabisa kuna vitu fulani nakosa, ninaomba msamaha kwake kama mzazi mwenzangu ilimradi kila kitu kiwe sawa kwa binti yetu. Kuna vitu nilikuwa nikivizingua na yeye anakasirika na Paula anajua kabisa hapa baba amekasirika.

"Lakini sisi kimbilio letu lilikuwa Samira ambaye ni mke wa Majani ambao wengi hamumjui wapo miaka mingi na wana watoto watatu, sisi tunampenda kwa sababu mimi na Paul tumeblokiana kila sehemu hatuongeagi lakini kimbilio langu tukiona kuna kitu kimefikia shingoni tunataka msaada kwa ajili ya Paula tanamfuata Samira tanamuelezea na atafikisha ujumbe kisha kila kitu kinakuwa sawa kwa hiyo mimi namshukuru sana na ninampenda sana," amesema Kajala.

Hata hivyo, kwa upande wake Majani amempongeza Paula na Marioo kwa hatua waliyofikia na kuwataka wawe mfano mzuri kwa watoto wao.

 "Ningependa kumwambia Omary (Marioo), sisi Aprili 19 tunatimiza miaka kumi katika ndoa yetu naomba na ninyi muweze kudumu muwe mfano mzuri kabisa kwa sababu tunategemea watoto wengine wengine,"amesema Majani.

Ikumbukwe kuwa mwanamuziki Marioo na mpenzi wake Paula Majani ambaye ni mtoto wa Kajala na Majani wanatarajia kupatapa mtoto wa kike.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags