Kago awachimba biti wanaotumia msemo wake, Afunguka bifu lake na mavokali

Kago awachimba biti wanaotumia msemo wake, Afunguka bifu lake na mavokali

Naam, tumekutana tena katika jarida letu pendwa la Mwananchi Scoop kwenye segment ya Burudani.

Miaka ya hivi karibuni imekuwa kawaida vipaji vingi kuibuka, kutoka na utandawazi vijana wengi nchini wamekuwa mstari wa mbele katika kuvitambulisha vipaji vyao kupitia mitandao ya kijamii.

Na hivyo ndivyo imetokea kwa muigizaji wa vichekesho ambaye amejizolea umarufu  mkubwa kupitia kikundi cha vichekesho ‘Cheka Tu’,  si mwingine ni Theodoro Emmanuel maarufu kama Kago.

Kama umewahi kusikia au kuutamka msema wa ‘Bado hujasema’ basi fahamu kuwa ndiyo msemo wake. Kabla ya kuingia katika tasnia ya burudani ya kuchekesha Kago alikuwa  mwanafuzi wa chuo cha TIA akisomea  Bachelor Degree in Public Sector Accounting and Finance (BPSAF).

Lakini alitamani kufanya vichekesho kwa kutafuta vikundi mbalimbali vya sanaa ili aweze kuonesha kipaji chake.

UGUMU KATIKA HARAKATI ZA UCHEKESHAJI

Wakati alipokuwa akijitafuta aoneshe kipaji chake haikuwa rahisi kwake, kutokana na kutokuwa na jina kubwa, na mtu wa kum-support kwenye sanaa.

Anasimulia kuwa alipata kazi sana mpaka kueleweka katika jamii juu ya kile anachokifanya,  kwa kutengeneza ‘clip’ na ku-post katika mitandao ya kijamii lakini haikufua dafu mpaka mwaka 2022 pale alipoamua kwenda katika kikundi maarufu cha vichekesho ‘Cheka Tu’ kinacho simamiwa na Coy Mzungu na kuanza rasmi kazi ya comedy.

“Kipindi naanza comedy ugumu ulikuwepo, nilipata kazi sana watu kuelewa ninachofanya, nilianza kwenye clip nikaona bado mapokeo ikabidi niende ‘Cheka Tu’, watu waelewe zaidi na hapo ndipo walipotambua uwezo wangu katika uchekeshaji” anasema Kago.

 UMUHIMU WA CHEKA TU KWAKE

Kago hakuishia hapo anaimbia Mwananchi Scoop jinsi Cheka Tu ilivyo na umuhimu kwake mpaka kujulikana na watu mbalimbali ndani ya tasnia na nje ya tasnia yaani mashabiki.

Pia anasema ilimvutia kwa sababu alianza kuifatilia tokea yupo shule akiwa hana mawazo ya kuchekesha,  alifuatilia kila hatua akiangalia watu wanavyo platform, anasema kuwa yeye anaona ‘Cheka Tu’ ndiyo platform mama kwa Tanzania.

“Cheka Tu ilinivutia kwa sababu nilianza kufatilia toka nipo shule sina hata mawazo ya kuchekesha, nilipenda tu watu wake wanavyo perform, tuseme tu ukweli ndiyo platform mama kwa Tanzania na imezalisha platform nyingine nyingi” anasema mchekeshaji huyo

 MAFANIKIO KATIKA VICHEKESHO (COMEDY)

Hata hivyo msanii huyo anaeleza kuwa comedy imempatia mafanikio makubwa mpaka sasa tofauti na alivyokuwa anajitafuta, pia anasema hawezi kuelezea wingi wa pesa alizopata kupitia uchekeshaji.

“Pesa nilizopata kuipata comedy ni nyingi siwezi kusema ni shilingi ngapi ila nimeweza kuwekeza na kuisaidia familia yangu kupitia kipato change ninachopata kwa sababu ya sanaa yangu” anasema Kago

Kipaji chake kimemuwezesha kumiliki kipande cha ardhi na kuwa na mipango ya kujenga katika kiwanja hicho akiamini ipo siku atakuja kumiliki nyumba yake kupitia talanta yake ya uchekeshaji.

NAMNA ANAVYOTENGENEZA CONTENT ZAKE

Kago anasema hana muda maalum wa kuandaa content  kwa sababu ni maisha yake ya kawaida anayoishi kila siku na huwa anatembea na note book ambayo akiona sehemu kuna kitu kinafaa kuwa contents huwa anaandika.

“Kwa upande wangu mimi naandaa content muda wote kwa sababu ni maisha yetu ya kawaida kwa hiyo kwenye simu yangu nina note book popote nitakapoenda nikiona hii ni content naandikia kisha nakuja kukaa na team yangu tunajadili vipi tuiweke kwenye ku-shoot” anasema Kago

CHANZO CHA MSEMO WA ‘BADO HAUJASEMA’

Kago anasema msemo wake ambao mpaka sasa unasikika kila kona na watu huutumia kama misemo mingine ‘bado haujasema’ ulianza wakiwa location team nzima baada ya rafiki yake wa karibu kuongea na simu akimwambia aliyekuwa naongea naye kuwa bado hajasema ndipo Kago alisikia akaona huo msemo anaweza kuutumia katika content.

“Msemo wa ‘bado hujasema’ ulipatikana pindi tulikuwa location nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Prosper Maulus alikuwa anaongea na simu akawa anamwambia aliyekuwa anaongea naye kuwa bado hujasema, ndiyo nikaona ina kitu nikaanza kuitumia”

UPEKEE WAKE KWENYE UCHEKESHAJI 

Yeye anajiona yuko tofauti na wachekeshaji wengine kutokana namna anavyo-host kwenye clip na jukwaani kwa sababu anaamini kila mchekeshaji ana shabiki yake ambaye anapenda style yake anapokuwa jukwaani.

“Kwenye comedy najiona wa pekee kwa sababu ninakitu cha tofauti na wengine kwenye upande wa uchekeshaji, ujue kila mtu ana namna ya uchekeshaj wake pia najiona wa pekee kwa sababu nafanya comedy kwenye ‘clip’ na stejini, nashukuru Mungu pande zote nafanya vizuri”. Anasema mchekeshaji huyu

KUZINGUANA NA  MAVOKALI

Hivi karibuni kulitokea sintofahamu ya masanii wa Bongo fleva, Mavokali kuchukua msemo wake wa ‘bado haujasema’ na kutumia katika wimbo wake, kutokana na hilo Kago alidai kuwa msanii huyo alichukua msemo wake bila ruhusa yake.

Kago amefafanua kuwa ilikuwa ni project ambayo waliandaa na msanii huyo iliku-push wimbo wa Mavokali.

“ Watu walishindwa kuelewa lile sakata la Mavokali kuchukua msemo wangu ilikuwa ni project ambayo iliandaliwa kwa ajili ya wimbo ”. Anasema Kago

Hata hivyo anasema kama kuna mtu akitokea anataka kutumia msemo wake anatakiwa afanye utaratibu wa kumtafuta waongee vizuri ili wafanye biashara kwa sababu msemo ameusajili kisheria.

Pia kupitia msemo wake amepata ma-deal mengi likiwemo Azam kwenye tangazo la Deby ya Simba na Yanga iliyofanyika Novemba 5,  2023.

VITU ASIVYOPENDA KWENYE MAISHA YA KAWAIDA

Kago ameweka wazi kuchukia dharau katika maisha yake hasa kwenye kazi zake, kama ikitokea mtu amemdharau huwa anaumia sana.

“Kusema kweli sipendi dharau, kwa sababu sijawahi kumdharau mtu yeyote kwahiyo akitokea mtu kanidharau naumia sana ila nitamuonesha kwa vitendo kwa kufanya kitu kizuri na baadaye atagundua kuwa alikosea kunidharau”. Anasema

KUHUSU NDOA NA MAHUSIANO

Inafahamika  Kago ameoa, lakini vijana wengi katika tasnia ya vichekesho wameonekana kutohamasika au kuonesha mahusiano yao hadharani lakini kwake imekuwa tofauti baada ya kuoa hivi karibuni.

Ameeleza kuoa ni uamuzi wa mtu na mwenza wake na yeye ameona ni jambo la kheri kwa kuwa limehalalishwa na Mungu hivyo kuoa ni kipaumbele chake.

 “Kuoa ni uamuzi wa mtu na huyo mwenza wake, mimi nimeona niliyenaye tumekubaliana na tunajuana vizuri tukaona siyo vibaya kuishi pamoja kwa halali.” Anasema

MPANGO WAKE WAKUFANYA SERIES

Kago katika kipaji chake anamipango mingi ya kufanya siku za usoni lakini kubwa zaidi ni juu ya mpango wake wa kufanya series kubwa ambapo ndani yake kutakuwa na kisa cha kuelimisha na kuburudisha,  anaamani jamii inayomzunguka itapenda.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags