Tattoo ni moja ya urembo ambao hufanywa na watu wa jinsia zote yaani wanawake kwa wanaume. Lakini tattoo si tu urembo kwenye mwili, bali ni njia ya kujieleza, kusherehekea kumbukumbu, au kuonyesha msimamo wa maisha. Hata hivyo, uamuzi wa kuchora tattoo haupaswi kufanywa kwa kukurupuka. Zingatia vitu hivi
- Maana ya Tattoo kwenye Maisha Yako
Tattoo nzuri huanza na swali "Kwa nini nataka tattoo hii?" Je, ni kwa sababu ya tukio maalum, kumbukumbu ya mtu , sanaa unayoipenda, au ujumbe?
Jiulize maswali hayo kwani Tattoos zenye maana huwa na thamani kwa mchoraji.
Epuka kuchora kwa shinikizo la marafiki, au kwenda na wakati.Hizi ndizo tattoo utazojutia baadaye.
- Chagua Sehemu Sahihi ya Mwili
Kila sehemu ya mwili huwa na maumivu yake. Maeneo kama mbavu, shingo, kifundo cha mguu huuma zaidi
Pia jiulize unataka Tattoo inayoonekana au iliyojificha. Tambua maeneo kama vidole au nyayo, ambayo hupata misuguano tattoo hufifia haraka.
- Pata Mchoraji wa Tattoo Anayeaminika, zingatia mambo haya kabla haujachora. Ana leseni au anafanya kazi katika studio halali?. Studio ni safi na ina vifaa vya kisasa?
Ana portfolio (picha za kazi alizofanya)?. Wateja wake wa zamani wanasema nini kumhusu?
Tambua hayo kwani uchaguzi mbaya wa mchoraji unaweza kusababisha maambukizi ya ngozi au maumivu yasiyo ya lazima
- Jitayarishe Kimwili na Kisaikolojia . Kabla ya siku ya kuchora kula vizuri, kunywa maji ya kutosha, va’a nguo rahisi kufungua eneo la tattoo, pumzika vya kutosha
- Fikiria Maisha ya Baadaye,tattoos ni za kudumu. Kabla ya kuchora
- Fikiria je, nitaipenda hii tattoo hata baada ya miaka 10?
- Je, itaniathiri kazini au kwenye familia/jamii ninayoishi?
- Je, ina alama au ujumbe usioeleweka vibaya katika tamaduni au dini fulani?
Ikiwa una mashaka, chora tattoo ya muda (henna) au tumia app ya kutest design kwenye ngozi yako kwanza.
- Uangalizi Baada ya Tattoo (Aftercare). Baada ya kuchora, msanii atakupa maelekezo,hivyo zingatia kila utachoambiwa ili uepuke maambukizi.
Leave a Reply