Jux aweka wazi tofauti ya Priscilla na wapenzi wake wa nyuma

Jux aweka wazi tofauti ya Priscilla na wapenzi wake wa nyuma

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini anayetamba na ngoma ya ‘Ololufemi’ Jux ameweka wazi tofauti kati ya mpenzi wake wa sasa Priscilla Ajoke na wapenzi wake wa nyuma kwa kueleza kuwa mpenzi wake huyo hana skendo zozote mbaya na amepokelewa kwa ukubwa ukweni.

Jux ameyasema hayo kwenye moja ya mahojiano yake aliyoyafanya mapema leo Jumanne Novemba 26, 2024 akieleza kuwa haimaanishi kama mahusiano yaliyopita hayakuwa bora lakini kwa Priscilla ni tofauti na wengine.

“Naweza nikasema unajua kila unaopokutana na watu wanautofauti na mimi nasemaga kwenye maisha hakuna kufeli kunakujifunza yaani mimi nikikosea kitu basi kwangu najua kama ni kitu cha kujifunza, pia namshukuru sana Mwenyez Mungu mahusiano yote, wasichana wote nimeshawahi kuwa nao nyuma kila mtu alikuwa na faida yake na kuna kitu alinipa na kujifunza pia kwahiyo siwezi nikasema hamna mtu yoyote alikuwa zaidi ya mwenzake”

“Lakini kwa huyu tofauti nadhani hata watu wamepokea sana kwa sababu nadhanu useriuos umeonekana hata kwa familia pia unajua katika mitandao nilionekana mimi kwao nilivyopokelewa na familia kitu ambacho sijawahi kupokelewa before na huku pia alivyokuja hata familia ilimpokea na unajua madada wanajua wakimuangalia mtu wanajua especiall wazazi wetu upande wakike kama akina mama wanajua kwahiyo walivyokaa nae kwa muda ndio maana unaona upendo wao ulikuwa mkubwa zaidi” amefunguka Jux

Mbali na hilo ameweka wazi kuwa binti huyo amemvutia zaidi kufuatia na kupambana kwenye biashara na uigizaji.

“Nadhani hicho ni kitu cha kwanza cha pili pia yule binti nilikuwa sijui kuwa ni mtu ambaye alikuwa akifuatiliwa na wasichana wadogo kwa sababu nayeye ni mdogo sana ana miaka 23 lakini vitu anavyovifanya hata nchi kwao anapendwa kwa sababu ni msichana mdogo lakini vitu vyake vinawapendeza watu wengi hana maskendo, anajituma anafanya biashara ameanza kuigiza mdogo unaiona cv yake ilivyo nzuri, kingine nadhani ananyota ya watu kuvutiwa naye” amesema Jux

Mahusiano ya wawili hao yalianza mapema mwezi Agosti huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandano ya kijamii ya ndani na nje ya Tanzania baada ya Jux kwenda ukweni nchini Nigeria.

Ikumbukwe kabla ya Jux kuwa kwenye mahusiano na Priscilla, alikuwa na Karen Bujulu. Priscilla Ajoke Ojo alionekana kwa mara ya kwanza na Jux July 19,2024 kwenye moja ya kumbi za starehe zilizopo jijini Dar es salaam.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags