Na Magreth Bavuma
Ouyah eeh! mambo niaje, hopefully wote tuko poa kabisa karibu tena kwenye corner yetu pendwa ya wanavyuo usisahau kuwaambia na wanao kwamba ujanja ni kuwa sehemu ya hii dunia yetu “uniconer”.
Afya ya akili ni suala linalokua kwa kasi miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Kulingana na utafiti wa mwaka 2021 uliofanywa na Chama cha Afya cha Vyuo Vikuu vya Marekani (ACHA), 61.6% ya wanafunzi wa vyuo vikuu walijihisi wamelemewa na kila kitu katika maisha yao mwaka uliopita, na 41.1% walijihisi wamehuzunika sana hadi ilikuwa vigumu kufanya kazi.
Utafiti wa mwaka 2020 uliofanywa na National Alliance on Mental Illness (NAMI) uligundua kuwa 75% ya matatizo ya afya ya akili huanza kabla ya umri wa miaka 24.
Utafiti wa mwaka 2021 uliofanywa na Chama cha Afya cha Vyuo Vikuu vya Marekani uligundua kuwa 40.7% ya wanafunzi wa vyuo vikuu walijihisi kuwa na ugonjwa wa akili katika maisha yao.
Utafiti wa mwaka 2022 uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) uligundua kuwa mmoja kati ya vijana saba wenye umri wa miaka 10-19 duniani kote ana ugonjwa wa akili.
Kumekua na matukio mengi ya kusikitisha kutoka kwa wanavyuo wenzetu ikiwemo kujirusha kutoka juu ya maghorofa, baadhi yao kunywa sumu na kukatisha ndoto zao, wapenzi kutoana uhai na mengine mengi yakusikitisha na yaliyoacha pengo kubwa na machozi mengi ya uchungu kwa familia na jamii kwa ujumla.
Kuna sababu kadhaa zinazochangia matatizo ya afya ya akili kwa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo wa masomo, wasiwasi wa kifedha, matatizo ya mahusiano, na upweke. Vyuo vikuu vinaweza kuchukua jukumu muhimu katika kuwasaidia wanafunzi wao katika kupambana na tatizo la afya ya akili kwa kutoa rasilimali na huduma zinazosaidia wanafunzi kukabiliana na changamoto hizi.
Kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafikia ushauri wa kisaikolojia na tiba ya afya ya akili ambayo inaweza kufanywa kupitia vituo vya ushauri vya vyuoni, au kwa kuwapa wanafunzi usaidizi wa kifedha kuomba ushauri kutoka kwa watoa huduma wa kibinafsi.
Vilevile kupitia kutoa semina na programu za elimu kuhusu afya ya akili inaweza kuwa njia mojawapo ya kusaidia wanafunzi kujifunza kuhusu masuala ya afya ya akili, jinsi ya kutambua ishara na dalili za changamoto ya maisha na jinsi ya kukabiliana na msongo wa mawazo na wasiwasi.
Kukuza utamaduni wa ufahamu juu ya afya ya akili kupitia kampeni na matukio ambayo yanaongeza ufahamu wa masuala hayo na kupunguza unyanyapaa.
Lakini pia walimu na wafanyakazi wengine wa vyuoni wanapaswa kufundishwa kuhusu afya ya akili ili kuwawezesha kutambua dalili na changamoto zinazojitokeza kwa mtu mwenye shida ya afya ya akili.
Kuhakikisha uwepo wa vikundi vya kusaidiana chuoni kunaleta nafasi ya wanafunzi kushirikiana na wenzao. Makundi hayo yatasimama kama msaada na faraja pale mtu anapopata nafasi ya kutambua kuwa hayuko pekeyake na kuna watu wenye changamoto kama yake.
Uongozi wa wanafunzi wa vyuo unatakiwa kuhamasisha uwepo wa michezo na mazoezi ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa endorphins, ambazo ni homoni za furaha.
Kuhamasisha wanafunzi kujihusisha katika shughuli za kujitolea, kushiriki mafunzo ya ziada, au kujaribu vitu vipya ili kuepusha mtu kukaa idol na kupatwa na msongo wa mawazo ambayo husababishwa pia na upweke.
Pia vyuo vinaweza kusaidia wanafunzi kujenga maisha na mipango ya baadaye kwa kuwa sehemu ya kutoa ushauri kwa wanafunzi wao katika uchaguzi wa nini wanawaza kufanya, ili kuepusha vijana walioko vyuoni kufanya maamuzi yasio sahihi na kusababisha majuto.
Afya ya akili ni muhimu kama afya ya kimwili. Vyuo vina nafasi yake katika kudumisha afya ya akili ya wanafunzi wao lakini pia wewe kama mwanachuo una nafasi yako hakikisha unajiepusha na stress za hapa na pale. Kama ni mahusiano sijui mpenzi mara marafiki cut them off your mental health matters.
Na unapohisi una uhitaji wa msaada juu ya afya yako ya akili usisite kufanya hivyo huku ukijiambia tu kuwa kutafuta msaada ni ishara ya nguvu, siyo udhaifu. Hakikisha hakuna mtu hata wewe mwenyewe uruhusu acheze na afya yako ya akili.
Kwa leo niseme shukrani sana kwa kuendelea kufuatilia kona yetu pendwa ya dunia ya wanavyuo “unicorner” kama una mawazo yoyote kuhusu makala zetu usisite kutufikia kupitia ukurasa wa Instagram @mwananchiscoop au nifikie mimi moja kwa moja @mcmaggie19 until next time tchaaoooo!!!!!
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply