Jose Chameleone afunguka siri ya mafanikio yake

Jose Chameleone afunguka siri ya mafanikio yake

Mwanamuziki kutoka Uganda Joseph Mayanja maarufu Jose Chameleone amefunguka siri ya mafanikio yake yanayomfanya andelee kukubalika katika tasnia ya muziki kwa kuweka wazi kuwa siri kubwa ni kufanya kazi kwa bidii.

Chameleone ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mahojiano yake na BBC kwa kuwataka wasanii ambao wanafanya muziki mwaka mmoja harafu wanaacha kutokukata tamaa kwani siri kubwa ya kupata mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii.

“Siri moja ni kuwa na kazi nzuri, kipaji, bidi na kutokukata tamaa, wapo watu wengi ambao wanaingia kwenye muziki halafu baada ya mwaka mmoja wanaanza kuchoka, kwa upande wangu haiko hivyo mimi kama msanii ambaye ni muimbaji Napata hamu ya kuimba kila nikiona kipaza sauti,” amesema Jose Chameleone

Mbali na hayo mwanamuiziki huyo alitaja wimbo wake pendwa anaukubali na kuweka wazi kuwa ni ‘Mama mia’ ambao ndio uliomfungulia njia katika muziki huku akiuita mtoto wake wa kwanza.

Ikumbukwe kuwa Chameleone ametamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo Valuvalu, Shida za dunia, Jamila, Mama mia, Tubonge, Mamaa Wange na nyinginezo nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags