Jokic aweka rekodi ya kibabe Nba

Jokic aweka rekodi ya kibabe Nba

Mchezaji wa Denver Nuggets, Nikola Jokic ameweka rekodi mpya ya takwamu ndani ya msimu mmoja kwenye historia ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA akivunja rekodi ya gwiji Wilt Chamberlain.

Jokic ameweka rekodi hiyo baada ya kufunga points 35 kwenye mchezo dhidi ya Memphis Grizzles ambao Nuggetgs walishinda kwa points 122 kwa 109.

Points zimemfanya raia huyo wa Serbia kuwa mchezaji wa pekee kwenye NBA kufunga pointi 2,000, rebounds 1,000 na assist 500 katika msimu mmoja.

Licha ya majeraha ya muda mrefu kwa baadhi ya wachezaji nyota wa Denver kama Jamal Murray na Michael Porter Jr, Jokic ameisaidia Nuggets kufuzu hatua ya mtoano play-off msimu huu ikiwa ni kwa msimu wa nne mfululizo wanafuzu katika hatua hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags