Johnny ya Yemi Alade ilitoka kimakosa

Johnny ya Yemi Alade ilitoka kimakosa

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Yemi Alade amefichua wimbo wake uitwao ‘Johnny’, ulitoka kimakosa, kwani haukupangwa kutoka kwa wakati huo.

Yemi wakati akifanya mahojiano na 'Podikasti' ya TeaWithTay ameeleza kuwa wimbo huo hakutaka utoke kipindi hicho bali ulivuja kupitia mitandao ya kijamii ndipo akaamua kuuachi.

Video ya wimbo wa ‘Johnny’ iliachiwa miaka tisa iliyopita na hadi sasa tayari umefikisha watazamaji zaidi ya milioni 160 kwenye mtandao wa YouTube. Yemi anatamba na ngoma nyingine kama vile Mama Afrika, Oh my gosh,Lipeka na shekere.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags