John Gotti afanya fujo ulingoni

John Gotti afanya fujo ulingoni

Usiku wa kuamkia leo katika pambano dhidi ya Floyd Mayweather na John Gotti III lilofanyika Florida nchini Marekani lilisitishwa baada ya uamuzi tata kusababisha vurugu kubwa katika ulingo.

Vurugu hiyo imetokea baada ya Mayweather kuanza mchezo huo kwa nguvu hiyo ni baada ya kuonekana kuchukizwa na mpinzani mwenzie Gotti wakati wa kupima uzito baada ya utani mwepesi, akianza kwa kasi ambayo hajawahi kuonesha katika mapambano mengine yaliopita.

Akionekana kutokupunguza kasi yake kwa muda wote wa pambano, akimshambulia mpinzani wake kwa nguvu ambazo zilifanya pambano lionekane linaweza kusimamishwa.

Mchezo huo wa ndondi uligeuka kuwa zaidi ya WWE Royal Rumble kuliko mechi ya kawaida wakati ulingo ulipoingia kwenye vurugu katikati ya raundi ya sita.

Sambamba na vurugu hiyo ilisababisha walinzi kutokea katikati ya umati wa watu na nyuma ya ulingo, lakini mpaka sasa haijulikani idadi ya majeraha yaliyosababishwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags