John Cena na mpango wa kustaafu mieleka

John Cena na mpango wa kustaafu mieleka

Mwanamieleka na muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani, John Cena ameweka wazi kuwa ana mpango wa kustaafu kucheza mieleka kabla hajatimiza miaka 50.

Cena ameyasema hayo wakati alipokuwa akifanyiwa mahojiano na ‘Entertainment Tonight’ na kusema mwaka huu 2024, anatimiza miaka 47, hivyo basi katika miaka mitatu iliyobaki anafikiria kustaafu kutokana na umri wake kumtupa mkono.

Aidha miaka kadhaa iliyopita, Cena alinukuliwa akisema kama atakuja kustaafu mieleka basi ni kutokana na viwango vya mchezo huo nchini humo kuwa vya chini.

John Cena amekuwa bingwa wa dunia mara 16, bingwa wa WWE mara 13, bingwa wa Dunia wa uzani mkubwa mara tatu. Bingwa wa WWE wa Marekani mara tano na mataji mengine.

Kati ya movie alizocheza ni Freelance, The Wall,Trainwreck,The Suicide Squad, Sisters, Blockers, Playing with Fire na Hidden Strike.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags