John Cena apanda jukwaani mtupu

John Cena apanda jukwaani mtupu

Mwanamieleka na muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani John Cena, amewaacha hoi wageni waalikwa kwenye utoaji wa tuzo za Oscar zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, Machi 10, nchini Marekani, baada ya kupanda jukwaani akiwa mtupu.

Cena alipanda jukwaani hapo wakati alipokwenda kumtaja mshindi wa Tuzo ya Mbunifu Bora wa Mavazi, ambapo mtangazaji wa tuzo hizo Jimmy Kimmel aliweka wazi kuwa muigizaji huyo huenda alifanya hivyo kwa lengo la kuwakumbusha watu kuhusiana na tukio kama hilo kuwahi kutokea katika usiku wa tuzo za Oscar.

Miaka 50 iliyopita katika usiku wa Tuzo za 46 za Oscar, 1974 muigizaji David Niven alipanda jukwaani akiwa mtupu wakati wa kumtambulisha Elizabeth Taylor.

John Cena ameonekana kwenye filamu kama ‘Freelance’, ‘Ricky Stanicky’, ‘The Marine’, ‘Argylle’ iliyotoka mwaka huu na nyinginezo, pia amewahi kuwa bingwa wa dunia mara 16, anashikilia rekodi bingwa WWE mara 13 ubingwa wa Dunia wa uzani wa juu (toleo la 2002-2013), mara tatu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags