Jiwe la kale lenye maandishi lililopotea larudishwa, Iraq

Jiwe la kale lenye maandishi lililopotea larudishwa, Iraq

Waswahili wanasema cha kale ni dhahabu msemo huo umethibitika huko nchini Iraq baada ya kupatikana kipande cha jiwe chenye umri wa miaka 2,800 kimeonyeshwa baada ya kurejeshwa kutoka nchini Italia kufuatia takriban miongo minne.

Mamlaka ya nchini Italia iliikabidhi kwa Rais wa nchi hiyo Abdul Latif Rashid katika mji wa Bologna wiki iliyopita.

Aidha bado haijabainika jinsi kibao hicho cha jiwe kilipatikana au jinsi kilivyofika Italia ambapo kilinaswa na polisi katika miaka ya 1980.

Waziri wa utamaduni nchini humo Ahmed Badrani alisema kuwa huenda kilipatikana wakati wa uchimbaji wa kiakiolojia wa bwawa la Mosul, ambalo lilijengwa wakati huo.

Kupitia hilo imeonyesha uporaji wa vitu vya kale nchini humo umeongezeka kufuatia uvamizi ulioongozwa na Marekani miaka 20 iliyopita.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post