Jinsi ya kutengeneza Scrub ya Kahawa

Jinsi ya kutengeneza Scrub ya Kahawa

Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, basi hapo kwenye kazi iendelee, Mwananchi Scoop imekuletea mbinu za kibishara zitazofanya ujipatie maokoto kila kukicha.

Kama inavyofahamika, kwa sasa watu wengi wamekuwa wakizingatia afya ya ngozi zao na kuzifanyia mambo mbalimbali ikiwemo scrub.  Hivyo basi kutokana na hilo wiki hii tumekusogezea namna ya kutengeneza scrub ya kahawa.

 

Mahitaji

  • Kahawa nyeusi au ya brown (inasaidia kuondoa michirizi kwenye ngozi ya binadamu)
  • Sukari ya brown (inasaidia kuondoa makovu na ngozi iliyofifia)
  • Mafuta ya nazi, ukikosa unaweza kutumia mafuta ya Mzaituni au mafuta ya Parachichi
  • Mafuta ya perfume harufu yoyote unayopendelea, na haya yatakusaidia kufanya scrub yako inukie vizuri.

 

Nb: kabla haujaanza kuwauzia watu unatakiwa kutengeneza scrub hiyo hata mara tano au zaidi vilevile kuitumia mwenyewe ili kujua ni kipi uongeze na kitu gani upunguze ili kisiweze kumletea madhara mtumiaji.

 

Namna ya kutengeneza

Chukua sukari yako na uiweke kwenye bakuli kubwa kiasi, hapa inategemea na kipimo ulichoweka lakini zangatia sukari isizidi. Mfano chukua vijiko 6 vikubwa vya sukari na uweke kwenye bakuli lako.

Kisha chukua vijiko sita au saba tena vya kahawa yako na uweke kwenye sukari yako,  uanze kwa kuchanganya sukari pamoja na kahawa mpaka mchanganyiko wako utakapochanganyika vizuri.

Kisha chukua mafuta  ya nazi na uweke kwenye mchanganyiko wako hapa sasa utaweka vijiko sita, kwa sababu ukiweka mafuta mengi scrub itakuwa na maji maji sana na siku zote scrub inatakiwa kuwa na unyevu kiasi.

Baada ya hapo utachanganya kwa muda kidogo mchanganyiko wako wa sukari, kahawa na mafuta ya nazi na ukiona uko sawa weka matone kadhaa ya mafuta ya perfume kwa ajili ya harufu.

 

Kama unahitaji scrub iweze kutoa povu basi utatakiwa kutumia ‘G acid poder’ vilevile unaweza kuongezea Liwa, na asali ili kufanya scrub yako kufanya kazi vizuri katika ngozi ya mtumiaji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags