Jinsi ya kutengeneza murtabak kwa ajili ya biashara/futari

Jinsi ya kutengeneza murtabak kwa ajili ya biashara/futari

Na Aisha Lungato

Alooooh! tulikubaliana kuwa mwendo ni ule ule wa kupeana tips za Ramadhani na leo nimewasogezea kitafunwa ambacho hakina mambo mengi, lakini ukila kwa ajili ya futari kitakufanya u-enjoy.

 Kwa wafanyabiashara hii ni nzuri sana ambayo itakufanya upate maokoto ya kutosha katika kipindi hiki, kama tunavyojua Ramadhani ipo mwishoni so wewe kama mfanyabiashara unatakiwa usizubae changamkia fursa .

 

Murtabak ni kitafunwa ambacho hutengenezwa kwa nyama ya kusaga, mayai pamoja na vitu vingine, kimekuwa kikiliwa sana. Bei yake huanzia shilingi 500 hadi elfu moja.

 

 

 

Mahitaji

      Nyama ya kusaga nusu kilo

      Manda ya duara au pembe nne

      Mayai 5 mpaka 8

      Pilipili mtama robo kijiko ( au unaweza kuweka upendavyo)

      Chumvi kiasi

      Karoti, Hoho, Kitunguu maji, pamoja na kitunguu swaumu

      Ndimu au limao

Manda unazotakiwa kutumia inabidi utengeneze mwenyewe na hazina utofauti na zile za sambusa lakini manda za Murtabak inabidi duara lake liwe kubwa kidogo.

 

Jinsi ya kutengeneza na kupika

      Chukua nyama yako ya kusaga weka kwenye sufuria, weka ndimu, kitunguu swaumu pamoja na pilipili mtama changanya

      Weka jikoni upike kwa moto mdogo ikiiva nyama yako waka pembeni na uache ipoe kidogo

      Chukua bakuli kubwa kiasi, kata vitunguu vidogo vidogo, karoti pamoja na hoho kisha gonga mayai yako lakini bakiza yai moja au mawili na ukoroge mpaka vichanganyike.

      Chukua flampeni weka mafuta kiasi kisha weka mayai yaive kwa moto mdogomdo (zingatia usiyageuze upande wa pili).

      Yakishaanza kukauka chukua nyama ya kusaga mwagia juu yote, acha vikauke kidogo na uepue

      Ukishamaliza chukua manda yako ya raundi au pembe nne itandike kwenye sinia kisha juu yake weka yale mayai  yenye mchanganyiko wa nyama ya kusaga.

      Kisha zungusha yaani ufanye umbo kama duara

      Anza kukata vipande utakavyo, kama nene au nyembamba ni wewe upendavyo.

      Ukimaliza kukata zote injika mafuta yako jikoni acha yapate moto.

      Chukua mayai mawili uliyoyaacha, yagonge weka chumvi kidogo na uyaweka pembeni

      Chukua Murtabark zako moja moja chovya kwenye yai uliloweka chumvi hakikisha yai linasambaa kwenye kona zote na utie kwenye mafuta.

      Zipike mpaka ziwe na rangi ya brown na uzitoe zitakuwa tayari kwa kuliwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post