Jinsi ya kutengeneza juisi ya Ndimu

Jinsi ya kutengeneza juisi ya Ndimu

Post Desc

Ndimu ikitumiwa kila siku huweza kupunguza uwezekano wa mtumiaji kupatwa na ugonjwa wa kupooza. Hii ni kwa mujibu wa American Heart Association ya nchini Marekani.

Tukiachana na ndimu kusafisha ngozi na kupunguza makunyanzi ya uzee, utumiaji wa ndimu kila siku husafisha viungo vya ndani vya mwili na kuvifanya viwe na utendaji sahihi zaidi hasa figo, mapafu, moyo na ini na hivyo mtu kuwa na afya njema yenye kila ahadi ya maisha marefu pia.

Ndimu pia ina uwezo mkubwa wa kuuchangamsha mwili lakini ndimu huweza kuufanya mtiririko wa damu mwilini kuwa katika uwiano sawa muda wote na kukufanya uwe makini bila kuchoka kutwa nzima. 

Basi baada ya maelezo yote ya kujua baadhi ya faida za ndimu, kwenye migahawa kadhaa jijini baadhi ya wafanyabiashara wamemua kuchukua fursa ya kutengeneza juisi ya ndimu kama kiburudisho kwa wateja wao, basi bila kupoteza muda nipo hapa kukujuza jinsi ya kutengeneza kinywaji hicho ili uweze kuchukua suala hili kama fursa.

 

Mahitaji

  • Ndimu 3-5
  • Sukari kiasi, unaweza kuweka robo lakini ukawa unapima wakati wa kuweka kwenye juice yako
  • Maji ya baridi lita moja
  • Asali (hii hautaiweka kwa wakati mmoja utachagua uweke sukari au asali lakini usije ukaweka vyote kwa wakati mmoja).
  • Radha either vanilla au hiriki pia unaweza kuweka tangawizi (sio lazima).
  • Brenda la kusagia juisi

 

Hatua ya kwanza: Chukua ndimu zako zioshe vizuri na uzimenye, wakati unamenya jitahidi sana kuondoa zile tunda zilizopo kwenye ndimu zako kwani zitasababisha juisi yako kuwa chungu hapo baadaye. Lakini pia ni hiyari kumenya ndimu wengine hawamenyi lakini mimi huwa namenya.

Hatua ya pili: Baada ya kumenya na kuondoa tunda zilizopo kwenye ndimu zako basi anza kwa kukata kata ndimu zako vipande vidogo vidogo ambavyo vitakuwa vyepesi kusagika kwenye brenda. 

Hatua ya tatu: Chukua ndimu zako ziweke kwenye Brenda kisha weka sukari robo lakini kama sio mpenzi wa sukari basi weka kiasi, na baada ya hapo weka maji kidogo kabisa kama nusu kikombe na uanze kubrend juice yako. 

Hatua ya nne: Ukibrend ukamaliza basi chukua chujio lako ichuje juice yako vizuri, iweke kwenye jagi na baada ya hapo ongeza maji yako yaliyobaki (ile litamoja imimine kwenye mchanganyiko wako uliosaga wa limao na sukari).

 

Ukishamaliza hapo chukua vipande vya barafu weka kwenye jagi la juice yako ili iweze kupata baridi au unaweza kuiweka kwenye friji kama hauna barafu na mpaka kufikia hapo juice yako itakuwa tayari kwa ajili ya kunywa au kuuza.

 

NB: Mara nyingi juisi hii huanzia 2000 kwa glasi moja hadi 3000 kwahiyo ni wewe kuchagua kuangalia tamthilia nyumbani au kuchangamkia fursa hii.

riptions






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags