Juice ya ukwaju ni moja ya kinywaji kinachosifika kuwa na ladha nzuri. Tunda ukwaju lenye wingi wa Vitamin B, C, K na aina nyingine za madini yenye faida mwilini, linaweza kutengeneza juisi tamu, inayofaa kutumiwa kipindi hiki cha jua kali.
Wataalamu wa afya wanashauri unywaji wa glasi moja ya juisi ya ukwaju kwa siku ili kupata matokeo mazuri kwa afya mwili kwani Ukwaju hulinda mwili dhidi ya mafua, hupunguza wingi wa lehemu na kuimarisha afya ya moyo.
Na katika ngozi, ukwaju husaidia kuing'arisha, kuwa nyororo, huondoa weusi kwenye shingo na kutibu chunusi.
Na kama unavyojua kipindi hiki ni joto kali, sehemu yenye mzunguko wa watu wengi moja ya changamoto wanayoipitia ni kiu ukiwa kama kijana unayetafuta kitu cha kufanya yaani biashara kwa kipindi kichi juice ya Ukwaju inaweza kukuokoa.
Jarida la Mwananchi Scoop wiki hii limeangazia namna ya kutengeneza juice ya Ukwaju ambayo kwa kupindi hichi watu huuza Sh 1000 au 2000 kwa glasi moja
Mahitaji
- Ukwaju nusu (sehemu za kununulia huwa wanapima so utamwambia akupimie robo kwa ajili ya kuanzia)
- Sukari robo
- Hiriki
- Vanilla robo kijiko
- Unga wa ubuyu (ukipenda maana baadhi ya watu hawapendelei kuchanganya wanahitaji kunywa juice ya Ukwaju ikiwa yenyewe fresh)
Jinsi ya kutengeza
Chukua ukwaju wako uloweke na maji kiasi kama dakika 15-20 ukimaliza utoe na uanze kutoa punje zilizopo kwenye Ukwaju.
Baada ya hapo uchemshe kidogo hapa kuna njia mbili unaweza ukachemsha lakini pia unaweza ukausaga katika brenda na kuchuja kama kawaida.
Kama umeuloweka utauchuja na uweke sukari, hiriki na vanila lakini kama utakuwa umeuchemsha basi utatakiwa kuusubiri mpaka upoe ndio uweke hivyo viungo vyote.
Wakati wa kubrendi au kuchemsha weka maji yanayotoshea ukwaju wako na ukimaliza hapo utahifadhi juice yako kwenye kidumu na uweke kwenye friji mpaka hapo itakuwa tayari kwa ajili ya kunywewa na kuuzwa.
Leave a Reply