Tunajua kuwa moja ya vitu vinavyowasumbu wanafunzi wengi ni kusoma na kisha kusahau kile ulichokisoma au kufundishwa.
Kutokana na changamoto hiyo leo katika Karia tumeamua kukuletea njia mbalimbali za kusoma ambazo zitakusaidia na kukuwezesha usisahau.
- Penda unachosoma
Ukisoma kitu unachopenda kuna uwezekano mkubwa wa wewe kukumbuka. Ndio maana tunasisitiza kuchagua kozi ambayo unaipenda na ndipo uweze kusoma.
Jiulize ni nyimbo ngapi unaweza kuziimba, wala hukufanya bidii yoyote kuzikariri lakini zipo kichwani. Ni kwa sababu ulizipenda nyimbo hizo hivyo unaposima penda kile unachosoma, soma ukitabasamu, usikunje sura, elimu siyo vita.
- Kuwa na malengo wakati wa kusoma
Unapoanza kusoma jiulize kwanini ninasoma kitu hiki? Ukiweza kujua kwa nini umeamua kusoma kozi hiyo au masomo uliyoyachangua basi uwezi kusahau hata kidogo na itkaufanya ufahulu katika mitihani yako ya mara kwa mara.
- Jipime mwenyewe unaposoma
Unaposoma kuwa na kalamu na daftari, baada ya kila kipengele jipime ili kuona kama unakumbuka, kwa mfano kama unasoma mada ya fulani hakikisha kila unapomaliza jikumbushie bila kuangalia kwenye daftari lako.
- Rudia tena na tena
Ukirudia mara nyingi utakumbuka mara nyingi, hivyo basi usisome mara moja ukoana umemaliza, unapaswa kurudia rudi, pale unapofundishwa darasani isome mada hiyo, unapopata muda tena baadae nenda usome tena na unapotangaziwa mtihani soma tena.
Mada moja ukiirudia kuisima mara saba kwa vipindi tofauti tofauti huwezi kuisahau.
- Fanyia mazoezi ulichokisoma
Njia hii ni bora na inasaidia kukumbuka kwa haraka zaidi, kuna njia mbili za kufanyia mazoezi kile ulichokisoma
Kwanza ni kumfundisha mtu kile ulichosoma. Soma kisha muite rafiki anza kumfundisha ulichosoma.
Njia ya pili soma mada fulani kish ita mrafiki katika majadiliano ili kujadiliana kuhusu mada hiyo. Wakati wa majadiliano toa hoja zako kuhusu mada hiyo hapo utakuwa mefanyia mazoezi ulichosoma.
disney
i can
disney
i can