Jinsi ya kupika Tambi za nazi

Jinsi ya kupika Tambi za nazi

Mambo vipi mdau karibu kwenye ukurasa wa nipe dili na leo moja kwa moja tutaelekezana jinsi ya kupika tambi za nazi.

Kama unavyofahamu tupo ndani ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani hivyo basi chukua fursa hii kujifunza namna ya kuandaa tambi zako za futari.

Unatakiwa kucheza na fursa bwana au vipi? usije ukasema unashindwa kupika tambi kisa mafuta hapana nazi zipo karibu tuelekezane.

Mahitaji


Tambi - pakti moja
Tui bubu - kipimo cha kikombe cha chai
Sukari - kipimo cha mkono kiganja kimoja
Maji - kiasi
Hiliki - kiasi
Chumvi - kiasi

Maelekezo


Bandika maji jikoni acha yachemke chemchem, chambua tambi zako ziwe moja moja kisha zitie kwenye maji ya moja na uache zichemke.

Zikishachemka ipua sufuria ya tambi na uzichuje maji yatoke yote, kisha zioshe tena tambi zako na maji ya kawaida.

Baada ya hapo bandika tui bubu jikoni likisha anza kuchemka weka sukari na chumvi kidogo kisha koroga hakikisha unakoroga sana, onja sukari kama imekolea weka tambi ndani ya tui na uanza kuchanganya mpaka zote ziwe zimeingia tui, nyunyizia hiliki zako na uchanganye vizuri. Kisha acha ziivie vizuri kwa moto mdogo mdogo.


Angalia tambi zako na zitakuwa tayari kwa kuliwa ili kujifunza mambo mbalimbali ya kuhusu jikoni fuatilia website yetu www.mwananchiscoop.co.tz

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags