Jinsi ya kupika saga noti kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kupika saga noti kwa ajili ya biashara

Niaje niaje, watu wangu wa nguvu, kama mjuavyo kauli mbiu yetu ni kupiga kazi tuu bila ya kujali ni kazi gani uifanyayo maana siku hizi hakuna kazi za kiume wala za kike.

Sasa leo katika segment yetu ya biashara tunakusogezea kitafunywa ambacho kimetokea kupendwa na watu wengi cha Saga Note, najua wengi wetu tunakijua kwa kukiona tuu na si kwa jina ila taratibu tutaelewana.

Kitafunwa hichi bwana ukipate na chai ya maziwa, wallah utaona dunia yote hakuna kitu kitamu kushinda hicho, maana hata mapenzi hayaingii ndani hahaha (jokes). Basi sasa tuendelee, kitafunwa hichi kinaasili kama andazi hivi na bei yake ni kuanzia tsh. 500-1000 inategemea na sehemu unaponunua.



Japo mkate huu una mambo mengi kidogo ila naamini tutaelewana tuu hivyo hivyo, haya ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua dondoo za pishi hilo, kwanza kabisa kuna mahitaji mawili ya donge la chumvi na sukari

MAHITAJI
Mahitaji ya donge la chumvi
• Unga ngano kikombe kimoja
• Chumvi robo kijiko cha chai
• Hamira kidogo
• Samli kijiko kimoja kidogo
• Maji ya vuguvugu ya kukandia
• Iliki kiasi
• Yai moja {ukipenda}
Mahitaji ya donge la sukari
• Unga ngano kikombe kimoja
• Sukari vijiko 2
• Hamira kidogo
• Samli kijiko kimoja kidogo
• Maji ya vuguvugu ya kukandia
• Iliki kiasi
• Yai moja {ukipenda}
Namna ya kuandaa na kupika.
1. Kanda donge la chumvi kwa kutumia mahitaji yake yote hadi upate donge laini, kisha weka kando, kisha kanda donge la sukari kama ulivyofanya kwa donge la chumvi.

2. Sukuma kama chapati, chukua donge la chumvi weka chini, sukuma donge la sukari litandaze juu ya donge la chumvi, Sasa roll pamoja, kisha kata slices wacha iumke kisha choma kwa mafuta yalipata moto wa wastani.

3. Chemsha shira yako{sukari na maji} usiache ikanata ya kawaida tu siyo kama shira ya visheti, kisha tumbukiza saganoti zako kwa sukari, alafu zitoe, na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa na kuuzwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post